
Mwanza. Polisi mkoani Mwanza wamemuua jambazi mmoja baada ya kujibizana kwa risasi muda huu.
Kamanda
wa Polisi mkoani humo, Ahmed Msangi ambaye yuko kwenye eneo la tukio,
amesema katika tukio hilo, askari mmoja amejeruhiwa kwa kupigwa risasi
mguuni na jambazi huyo aliyeuawa ambaye alikuwa na mwenzake anayedaiwa
kukimbilia kwenye majabali ya mawe.
Amesema majibizano hayo yalianza saa 6.20 katika Mtaa wa Utemini, baada ya polisi waliokuwa doria kufuatilia nyendo za watu hao.
“Tulipokea taarifa kutoka kwa rai wema kuwa katika eneo hilo kuna watu wanaowatilia shaka, ndipo askari wakaamua kuwafuatilia.
Hata hivyo, amesema wamefanikiwa kukamata bastola moja iliyokuwa ikitumiwa na jambazi huyo.
“Unasikia
milio hiyo ya risasi, askari wanaendelea kumsaka huyo mmoja
aliyejificha kwenye mawe, naimani tutampata tu na hatuondoki hapa mpaka
tumtie mikononi,” alisema Msangi na kuongeza:
“Hawa
ni majambazi sugu ambao walikuwa wakituhumiwa kufanya matukio uporaji
na mauaji jijini hapa, tulikuwa tukiwasaka kwa muda mrefu.”
