» » PHIL NEVILE AMPIGA DONGO BALE BAADA YA USHINDI WA ENGLAND

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO
 Gareth Bale atajuta kutoa maneno ya kejeli dhidi ya England baada ya kushuhudia jana Wales ikinyolewa na England mabao 2-1.

Ikumbukwe kuwa kabla ya mchezo huo wa jana, Bale aliwatuhumu wachezaji wa timu ya England kukosa morali ya kuicheza timu hiyo, huku akijinasibu wao kuwa na umoja wa kupambana kwa ajili ya taifa lao.

Alienda mbali zaidi na kusema kwamba wanegewafunga England maarufu kama ‘Three Lions’ kutokana na ari ya kujituma iliyojaa kwa timu yao.

Lakini kitu kibaya zaidi ni kwamba walipoteza mchezo huo, sasa baada ya mchezo kumalizika, ndipo alipotamani kutumbukia ndani ta ardhi kuficha aibu kwenye uso wake.

Phil Neville ambaye ni beki wa zamani wa kulia wa Manchester United na England kupitia akaunti yake alimidhihaki Bale na kuposti ujumbe unaosomeka ‘No passion from England’ akimaanisha hakuna moyo wa kujituma kwa wachezaji wa England.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post