Microsoft kushiriki biashara ya Bangi
Kampuni hiyo kubwa imeungana na kampuni nyingine ya "Kind Financial - inayotengeneza
programu za kusaidia idara za serikali zinazodhibiti uzalishaji na mauzo ya bangi.
Kind Financial imekuwa ikiuza programu zake kwa idara za usalama zinazofuatilia ukuzaji uuzaji na usambazi wa bangi
Yamkini Microsoft inasema kuwa uhusiano wake na kampuni hiyo yenye makao yake makuu huko Carlifornia ni wa ''kipekee''
Kind Financial imekuwa ikiuza programu zake kwa idara za usalama zinazofuatilia ukuzaji uuzaji na usambazi wa bangi kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.
Microsoft imeungana na kampuni nyingine ya "Kind Financial
Programu hiyo ya Kind inaitwa ''Agrisoft Seed to Sale, " na inawaunganisha wakulima wa bangi wauzaji idara zinazosaidia kudhibiti matumizi ya bangi serikali na na sekta ya fedha.
Majimbo kadhaa nchini Marekani yameruhusu uuzaji wa bangi kwa matumizi ya kimatibabu na kujistarehesha, japo imeharamishwa chini ya sheria kuu za nchi hiyo.


