» » MASHABIKI SIMBA WAINGIA HOFU YA USAJILI, HANS POPPE AWAPA UFAFANUZI

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Mashabiki Simba wameanza kuingia hofu kwamba uongozi wao haufanyi lolote kuhusiana na usajili.

Hofu hiyo inaingia baada ya kuona Yanga ikiendelea kusajili mfululizo lakini wao wakiwa hawajafanya jambo.

Baadhi ya waliotuma maoni  wamekuwa wakilalama kwamba suala la usajili kwao linaonekana kwenda taratibu.

Wengine waliutaka uongozi wa Simba kuinua macho haraka na kuangalia uwezekano wa kufanya usajili sahihi.

Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema kila kitu kinaendelea kwa mpangilio.

“Kila kitu kinakwenda vizuri, hatuna sababu ya kuwa na haraka. Yanga wanakwenda na mipango yao na sisi tuna yetu.

“Wao wanaanza maandalizi sasa, sisi muda bado. Lakini si kweli tumekaa tu na si kila tunachofanya kitangazwe,” alisema.

Tayari Hans Poppe alishasafiri hadi Zimbabwe ingawa alisema ni masuala yake binafsi, lakini alishughulikia masuala ya usajili pia.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post