Imeelezwa kuwa idadi kubwa ya wanawake ni nguzo kuu katika kufanikisha kufikiwa kwa malengo ya maendeleo ya dunia kama vile upatikanaji wa huduma za afya na elimu, maji safi na salama, usafi na utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi imara na kwamba hayo yanaweza kufanikiwa kama serikali zitaamua kutumia nguvu kazi hiyo muhimu.
Ikiwa ni miaka 20 sasa tangu kongamano la Beijin, licha ya wanawake kuunda asilimia kubwa ya nguvu kazi katika kilimo na ujasilia mali, bado wengi wanakabiliwa na vikwazo vingi kama vile masoko, ubaguzi, unyonyaji, mila potofu, kushindwa kumiliki rasilimali muhimu kama ardhi, na kushindwa kupata fursa za kifedha katika taasisi za kibenki, lakini makamo wa rais Mh.Samia Suluhu Hassan amesema bado wanawake ni kundi muhimu katika ujenzi wa uchumi wa dunia.
Serikali kupitia wizara ya maendeleo jinsia na watoto inasema imekiri kwamba bado haijatumia vema mchango wa asilimia 51 ya idadi ya wanawake wa Tanzania katika kujenga uchumi huku ikisema tayari imekwisha kuanza kutekeleza mipango ya kitaifa na ya kisecta ilikufanikiwa kuwa na usawa wa kijinsia na kiuchumi.
Katika kongamano hilo la uzinduzi wa kumuwezesha mwanamke kiuchumi, lililohudhuliwa na idadi kubwa ya wanawake wajasilia mali, mada mbalimbali zilitolewa zote zikilenga kumkomboa mwanamke kiuchumi.
Aidha katika kongamano hilo makamo wa rais amewataka wanawake kuhakikisha wanaheshimu fedha katika biashara zao, huku akiahidi kuhakikisha zaidi ya asilimia 30 ya tenda zote katika ngazi ya serikali za mitaaa kuelekezwa kwa wanawake wajasiliali ilikuwainua kiuchumi.