Kocha mpya wa Everton Ronald Koeman
Katika kuhakikisha inafanya vema katika michuano ya msimu ujao timu ya
Everton imefanikiwa kuimarisha benchi lake la ufundi mara baada ya
kuingia mkataba rasmi na aliyekuwa kocha wa Southampton Ronald Koeman.
Kocha huyo raia wa Uholanzi anachukua nafasi iliyoachwa na kocha Roberto Martinez ambaye alionyeshwa mlango wa kutokea baada ya kuwa na msimu unaosuasua na vijana hao wanaotumia dimba la Goodson Park.
Taarifa zinaweka wazi kuwa kocha Koeman amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kukinoa kikosi cha timu hiyo na anataraji kuingiza kitita cha paundi million 6, akilipwa kiasi cha paundi million 2 kila msimu kwa mujibu wa mkataba wake huo.

