» » Ilala yaanza kumsaka chatu wa Mto Mzinga

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Dar es Salaam. Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imedhamiria kumsaka nyoka aina ya chatu anayeishi karibu na Mto Mzinga ambaye amekuwa tishio kwa wakazi wa eneo la Lubakaya, Kata ya Zingiziwa.
Nyoka huyo amekuwa akionekana kati ya saa 12 hadi saa 1 jioni akitokea kwenye mto huo na kuelekea kwenye makazi ya watu kula mifugo, jambo ambalo linahatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo.

Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Isaya Mngurumi amesema chatu huyo alionekana mara moja, hivyo ofisi hiyo imetuma wataalamu ambao watashirikiana na diwani wa kata hiyo kumsaka

Mngurumi alisema mwanzo alituma watu kutoka kwenye halmashauri hiyo ambao walishirikiana na wananchi wa eneo hilo kumsaka chatu huyo lakini hawakufanikiwa.

“ Mwanzo niliagiza timu yangu ambayo walishirikiana na wananchi akiwemo diwani wa eneo hilo, lakini hawakumpata hivyo nimeamua kutuma wataalamu waweze kumsaka chatu huyo,” amesema.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post