» » Hanscana Direkta Kutoka kushika taa hadi kumiliki studio ya billioni 1

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Bongo ni vigumu kuwataja madairekta wanaotengeneza vichupa vikali na usimtaje Hanscana. Utakuwa unachekesha aisee maana jamaa huyu ambaye alibeba Tuzo za Watu mwaka 2015 katika kipengele cha Mwandaaji Bora wa Video yuko kwenye ubora wake.

Katika ‘exclusive interview’ na Risasi Jumamosi, Hanscana anafunguka moja kwa moja mambo mengi yanayohusiana na kazi yake.

Risasi Jumamosi: Una jina kubwa na wasanii wengi wanapenda kufanya kazi na wewe, unatoza shilingi ngapi kwa video?
Hanscana: Inategemea na ‘script’ inataka nini, kuna video zinahitaji gharama kubwa kutokana na mahitaji yake, hata hivyo hii ni biashara, kuna maelewano baina ya pande mbili.
Risasi Jumamosi: Sawa, unaweza kuwaeleza wasomaji ujuzi wako wa kutengeneza vitu vikali umeutoa wapi?
Hanscana: Kwa kweli ni stori ndefu, nime-hustle sana kwenye gemu kutafuta ujuzi nilionao leo. Nimeshika sana kamera na taa nikiwa lokesheni kwa madairekta wengine niliopitia mikononi mwao. Hata hivyo nilifanya hayo yote nikiwa na patient (uvumilivu) kuwa siku moja nitakuwa bora kama nilivyo leo.
Risasi Jumamosi: Dairekta gani unamzimia Bongo na kwa nini?
Hanscana:  Namkubali Nicklass aliyetengeneza Video ya Wimbo wa Shika Adabu Yako wa Nay wa Mitego. Si maarufu sana lakini anajua,upigaji picha wake pamoja na namna anavyochanyanga matukio ni hatari!
Risasi Jumamosi: Kipindi gani ambacho huwezi kukisahau kwenye kazi unayoifanya?
Hanscana: Nilipokutana na direkta kutoka Sauz, Justin Campos wakati alipokuwa Bongo kushuti video ya wimbo wa Diamond, Utanipendaga. Nilijifunza mambo mengi kutoka kwake.
Risasi Jumamosi: Maelewano na Nisher yako vipi? Na nini kilitokea hasa mpaka wewe ukafanya kazi na G Nako ambayo pia Nisher alikuwa amekwishaifanya?
Hanscana: Hakuna tatizo kati yangu na Nisher. Kuhusu ishu ya Wimbo wa Arosto wa G Nako, siwezi kujibu lolote, aulizwe G Nako.
Risasi Jumamosi: Unaweza kutaja kwa uchache wasanii ambao umepiga nao kazi Bongo!
Hanscana: Ni wengi sana siwezi kuwataja wote. Kuna Navy Kenzo, V- Money, Barnaba, G Nako, Linex, Malaika, Feza Kessy na Belle 9.
Risasi Jumamosi: Oke, si mbaya kama ukiweka wazi juu ya mafanikio yako kwa sasa!
Hanscana:  Namshukuru Mungu si haba. Napenda kuchukua fursa hii pia kuzungumzia studio iitwayo Wanene Films iliyopo Mikocheni B jijini Dar.
Ni studio ya kisasa iliyogharimu zaidi ya shilingi bilioni moja mpaka kufikia ilipo na tutaizindua soon. Mtu aliyei-design anatokea Ufaransa na mpaka sasa ame-design duniani studio 104, tatu zikiwa Afrika na moja wapo ndiyo hii. Lakini kampuni inayotengeneza inatoka Afrika Kusini.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post