Tuanze kuangalia picha 5 zinazotukumbusha tulipotokea katika sekta hii ya teknolojia
simu-za-zamani
Simu hizi za mezani zilijizolea umaarufu mkubwa sana katika kipindi cha
miaka ya 80′ na 70′ duniani. Zikiwa zinatumia waya katika kuonganisha
pointi moja na nyingine zilikuwa msaada mkubwa sana kwa kipindi hicho.
Ofisi za serikali na baadhi ya mashirika ndio walikuwa na uwezo wa kuwa
nazo.
tv
Televisheni za kutune kwa kipindi hicho zilikuwa katika ubora wake, kwa
nchini kwetu Tanzania watu wawili wa kwanza kumiliki Televisheni kwa
mujibu wa chanzo kimoja walikuwa ni Baba wa Taifa na Sheikh Yahya japo
haina uhakika sana kama walikuwa wanatumia aina hii ya Tv. Kituo pekee
cha TV kilikuwa kituo cha Televisheni cha Zanzibar.
mobile-phone
Simu za mkononi za kwanza kutumika nchini zilikuwa kubwa kama
zinavyoonekana katika picha nyingi zikiwa kutoka kampuni ya Siemens na
Motorola. Huku kukiwa na mtandao mmoja mkubwa wa simu wa Mobitel katika
baadhi ya maeneo ya mijini.
santuri
Santuri ni jina geni kwa vijana wengi wa kizazi cha sasa, ikiwa na uwezo
wa kuwekwa nyimbo mpaka za dakika 45 santuri ndio ilikuwa njia pekee ya
kusikiliza muziki maridhawa katika baadhi ya klabu nchini.
cassete
Redio za Cassette za kutembea nazo maarufu kama Walkman kwa kipindi
hicho zilikuwa zinabamba sana, kutoka kwenye walkman teknolojia
ikatupeleka katika mp3, iPod na mpaka sasa hakuna haja ya kuwa na vifaa
hivi kwa sababu 100% ya kazi zake zinafanywa na simu.





