» » Aliyeolewa bila ruhusa achomwa hadi kufa Pakistan

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Maafisa wa polisi katika mji wa Pakistan wa Lahore wamemkamata mwanamke anayetuhumiwa kumuua mwanawe wa kike kwa kufanya ndoa bila ruhusa ya familia.

Maafisa wa polisi wanasema mwili wa Zeenat Rafiq una ishara za alama za mateso.
''Alifungwa kamba katika kitanda ,kumwagiwa mafuta na kuchomwa''.

Mamaake anatahumiwa kwa kumchukua kutoka kwa wakweze.

Ni kisa cha tatu katika kipindi cha mwezi mmoja nchini Pakistan ambapo mashambulio ya wanawake wanaokiuka sheria za kihafidhina kuhusu mapenzi na ndoa hufanyika.

Wiki iliopita mwalimu Maria Sadaqat,alichomwa katika eneo la Murree karibu na mji wa Islamabad kwa kukataa kuolewa.

Alifariki kutokana na majeraha.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post