» » Aliyemtukana Rais akabidhiwa Sh4.5 milioni

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Arusha. Wanaharakati na wadau wa mitandao ya kijamii nchini wamemkabidhi Sh4.5 milioni aliyekutwa na hatia ya kumtukana Rais John Magufuli ili akaulipa faini aliyotakiwa atoe na mahakamani kuepuka kifungo cha miaka mitatu.

Mshtakiwa huyo, Isaack Habakuki alikutwa na hatia baada ya kukiri kosa la kumtukana Rais kupitia ukurasa wake wa facebook.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imemtaka kutoa Sh 7 milioni au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
Mratibu aliyekuwa anakusanya michango hiyo kwa Kanda ya Kaskazini,  Diwani wa Levolosi,  Ephata Nanyaro amesema jana kuwa  wamefanikiwa kupata michango hiyo kupitia makundi ya mitandao ya kijamii waliyoyaanzisha.

"Lengo ni kumsaidia mwenzetu kwa kuwa kupitia sheria hii ya mitandao tunaamini hakuna aliyesalama na sheria hii itawagusa wote, " amesema Nanyaro.

Naye,  Habakuki amewashukuru Watanzania waliojitolea kumchangia akisema kupitia adhabu hiyo atakuwa wa kwanza kufundisha jamii kuhusu sheria za mitandaoni
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post