» » Yanga na Azam FC kuonyeshana kazi leo Taifa

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Azam FC na Yanga wanakutana jioni ya leo katika Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo utachezeshwa na refa Israel Mujuni Nkongo wa Dar es Salaam, ambaye atasaidiwa na Ferdinand Chancha wa Mwanza na Soud Lila wa Dar es Salaam wakaopeperusha vibendera, wakati mezani atakuwapo Frank Komba wa Dar es Salaam pia na Kamisaa ni mshambuliaji wa zamani wa Kimataifa wa Tanzania, Juma Mgunda wa Tanga.

Kwa upande wa TFF imekwishaitangaza Azam FC itacheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, kwa kuwa Yanga tayari wana tiketi ya Ligi ya Mabingwa, hivyo fainali ya leo ya Kombe la FA itahitimisha msimu na kupata fursa ya kujua mbabe baina ya timu hizo.

Yanga inashuka uwanjani leo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuizidi Azam FC katika mataji mawili, ikiwa ni katika Ngao ya Jamii Agosti 22 mwaka jana waliposhinda kwa penalti 8-7 baada ya sare ya 0-0 na baadaye katika Ligi Kuu, ingawa timu hizo zilitoa sare mechi zote mbili, kwanza 1-1 Oktoba 17, mwaka jana na baadaye 2-2 Machi 5, mwaka huu.

Mchezo mwingine uliozikutanisha Yanga na Azam msimu huu ni wa Kombe la Mapinduzi ambao pia zilitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Ndani ya dakika 90, hakuna mechi ya Yanga na Azam FC imetoa mbabe msimu huu na mchezo wa leo kwa kuwa ni wa fainali, unaweza kufika kwenye mikwaju ya penalti pia.

Kwa mara ya kwanza msimu huu, Azam itakutana na Yanga katika bechi la Ufundi kukiwa na mabadiliko, baada ya kundolewa Muingereza Stewart John Hall na timu yake na kuajiriwa Mspanyola Zebensul Hernandez Rodriguez na timu yake.

Yanga itaendelea kuwa chini ya Mholanzi, Hans van der Pluijm ambaye alitaka kugombana na kocha wa Azam katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu Zanzibar.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post