» » Mkapa akanusha taarifa za kuwatenga wadau muhimu katika mazungumzo ya amani Burundi.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Mazungumzo ya kutafuta amani nchini Burundi yanayoendelea jijini arusha chini ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh benjamini Mkapa  leo yameingia katika siku ya tatu na ofisi ya msuluhishi huyo imetoa  ufafanuzi wa malalamiko ya baadhi ya wanaharakati ya kutoalikwa kwa  baadhi ya wadau muhimu katika mgogoro huo inayoonyesha kuwa wote  walialikwa lakini wengine hawakuweza kufika.

 Taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa  wadau wote muhimu vikiwemo vyama vya upinzani,taasisi za dini,na  wanaharakati vimealikwa na baadhi vilithibitisha kushiriki na vingine  havikutoa majibu  yoyote.

Aidha taarifa hiyo imeanisha baadhi ya vyama vilivyoalikwa na ambavyo  vimeweza kushiriki kuwa ni pamoja na CNDD/FDD Sahwanya Frodebu na Rodebu/Copa pamoja na marais wastaafu wa Burundi  Sylvestre Ntibantunganya na Domitien Ndayizeye na pia mwanasiasa maarufu nchini Burundi Agathon Ruasa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo vyama vilivyoalikwa na kushindwa   kushiriki ni pamoja na chama cha MSD na kwa upande wa viongozi ni pamoja na Rais mstaafu wa Burundi Pier Buyoya na kwamba jitihada za  kutafuta sababu za kushindwa kushiriki zinaendelea.

Hadi sasa tayari wajumbe wawakilishi wapatao 83 wa makundi yenye maslahi katika mgogoro huo wamefika Arusha  na wanaendelea na majadiliano.

Alipokuwa anafungua mjadala wa mazungumzo hayo mh Rais mstaafu Mkapa  aliwaeleza wajumbe wanaoshiriki kuwa wadau wote  muhimu wa mgogoro  huo wamealikwa.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post