
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Endwin Ngonyani amesema kwamba ukweli upembuzi yakinifu wa barabara hiyo umekamilika na serikali kwa sasa inatafuta fedha ili kuweza kujenga barabara hiyo kuanzia wakati wowote.
Naibu waziri huyo amekiri barabara hiyo kuwa kwenye ilani ya chama cha mapinduzi ukurasa wa 61 hivyo barabara hiyo itajengwa ili kuongeza kasi ya maendeleo katika ukanda huo.
-Aidha Mhandisi Ngonyani amesema kwamba TANROADS itaendelea kukarabati barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe hadi hapo fedha zitakapo patikana.
