» » Mayunga: Hakuna msanii aliyeniita tufanye collabo, labda wanaogopa

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO
Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars mwaka jana, Nalimi Mayunga ametoa sababu ya kuogoapwa na baadhi ya wasanii ndiyo imemfanmya asishirikishwe kwenye nyimbo za wasanii wengine.
4K0A7828
Kwa sasa Mayunga anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Please Don’t Go Away’ aliomshirikisha msanii kutoka Marekani mwenye asili ya Senegal, Akon. Akizungumza na Bongo5, Mayunga amesema kuwa bado hajaitwa na msanii yeyote kutoka Tanzania ili wafanye collabo.
“Bado sijafanya collabo yeyote na msasnii kutoka bongo na hakuna msanii yeyote mkubwa aliyenitafuta. Nafikiria watakuwa wanaogopa tu, mimi nipo tayari muda wowote kufanya nao,” aliongeza.
Aidha Mayunga amewatoa hofu mashabiki wake kwa kuwaambia kuwa bado kuna uwezekano mkubwa kwa yeye kufanya nyimbo nyingine mbili au hata zaidi na Akon.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post