» » Manispaa ya Musoma yakabiliwa na uhaba mkubwa wa Sukari

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Uhaba mkubwa wa Sukari katika manispaa ya Musoma umesababisha wananchi kutumia zaidi ya saa kumi katika foleni za kununua bidhaa  hiyo huku bei yake ikizidi kupanda kutoka shilingi elfu mbili hadi shilingi elfu tano kwa kilo moja ya Sukari.
Baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya rejareja wa mjini Musoma, wakizungumza huku wakiwa katika foleni hiyo katika moja ya duka lilokuwa likiuza bidhaa hiyo katika barabara ya sokoni mjini Musoma, wamesema wanalazimika kujipanga kwa zaidi ya saa kumi wakisubili kuuziwa mfuko mmoja wa Sukari wa kilo 50 kutoka nchini Brazil kwa  shilingi 130,000.
 
Hata uchunguzi ambao umefanywa na ITV umebaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wakitoa masharti na kuuza mfuko mmoja wa Sukari kwa shilingi 130,000 huku wakitoa stakabadhi za shilingi 105,000 kwa wauzaji hao wa rejareja.
 
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post