Kampuni ya Nokia imerudi upya katika ulimwengu wa ushindani wa simu za
Smartphone zenye mfumo wa android baada ya wiki hii kuingiza sokoni simu
mpya aina ya Nokia 6 na kuuzika kwa muda wa dakika moja.
Nokia kwa sasa ipo chini ya kampuni ya HDM Global na liliuza simu za
Nokia 6 huko nchini china tuu na ndipo walipopata matunda makubwa.
Mauzo ya simu hii yalifanyika katika mall ya JingDong, na watu ambao walijiandikisha mwanzoni kabisa kabla hata ya simu haijafika hapo ili ikifika wawe wakwanza kuipata walikua ni zaidi ya milioni moja na laki tatu.
Japokuwa haijulikani kwa undani kuwa Nokia iliuza simu ngapi ndani ya dakika hiyo moja lakini kinachojulikana ni kwamba ziliisha zote ambazo zilikuwa katika stoo.
Nokia ilikua inauzika china kwa gharama ya yuan 1699 ambayo ni ni sawa na dola 248 za kimarekani na kwa haraka haraka ni sawa na laki tano za Tanzania.
Pengine sifa za simu hii ndio zimeipa umaarufu mkubwa ukiachana na kuwa kampuni ya Nokia kwa kipindi cha muda mrefu imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa inatengeneza simu ambazo ni imara na zinazodumu kwa muda mrefu.
Source: Gsmarena/Teknokona