» »Unlabelled » 7 mbaroni kwa upatu wa sh mil 100/-

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

WATU saba wamekamatwa mkoani Mwanza akiwemo mwanamke mmoja ambaye ni mmiliki wa Kikundi cha AQ Power Club kwa tuhuma za kuwaibia wananchi fedha kiasi cha shilingi milioni 100 baada ya kuwashawishi kujiunga na biashara ya upatu, kwa madai ya kuwekeza fedha kidogo ili baadae walipwe fedha nyingi na kikundi hicho.

Kamanda wa polisi, mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi alimtaja mwanamke huyo kuwa ni Happy Aloyce ( 35) Mkazi wa Mtaa wa Ilemela eneo la Mahakamani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni binafsi ya AQ Computer Limited.

Alisema hivi karibuni kumejitokeza wimbi kubwa la vikundi vinavyo watapeli wananchi mkoani Mwanza, kikiwemo cha mwanamke huyo na wenzake waliokamatwa ambao baadhi yao wamepora fedha za wananchi kupitia njia ya udanganyifu ya upatu.

Kamanda Msangi alisema kuwa mwanamke huyo na watu aliokuwa anashirikiana nao wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 100 kutoka kwa wananchi aliowashawishi wajiunge na kikundi chake.

“Upelelezi wetu umebaini kuwa AQ Club sio taasisi iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria bali ni jina la biashara la mtuhumiwa… huyu mtuhumiwa na wenzake saba ( majina yanahifadhiwa) wamekamatwa na upelelezi unaendelea na utakapokamilika jalada litapelekwa kwa Mwanasheria wa serikali kwa hatua zaidi za kisheria dhidi yao,” alisema.

Kamanda Msangi ametoa tahadhari kwa wananchi wote wa mkoa wa Mwanza kuchukua tahadhari juu ya uwepo wa vikundi hivyo vinavyowatapeli wananchi kwa kuwaibia fedha zao kwa muda mfupi bila ya kufanya kazi.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post