» »Unlabelled » Wagonjwa 230 wafanyiwa upasuaji wa macho Dodoma

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Monday, December 12, 2016

Zaidi ya wagonjwa 230 Mkoani Dodoma wamefanyiwa upasuaji wa Macho na kupatiwa miwani katika zoezi lililoendeshwa na Bilal Muslim Mission iliyopo mkoani Dodoma.

Akizungumzia upasuaji huo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Caroline Damian, ameishukuru taasisi hiyo na kusema kuwa zoezi hilo limekuwa na tija kwa wakazi wa mkoa huo.

Naye Naibu Waziri nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi , Vijana na Ajira, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde ameshukuru kuendeshwa kwa zeozi hilo huku akitoa wito wa msaada zaidi wa matibabu kwa watu wasiojiweza mkoani humo.

Akizungumzia zoezi hilo Mganga aliyehusika katika upasuaji huo Dkt. Njau Sendgodry, amesema kutokana na ukubwa wa tatizo la Macho mkoani Dodoma amesema ni wakati muafaka sasa kwa hospitali zote mkoani humo kuwezeshwa ili kutoa huduma kikamilifu.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post