» »Unlabelled » Mkuu Wa Wilaya Ya Ubungo Alakiapo Leo Jijini Dar Es Esalaam

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimwapicha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisari Matiku Makori kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni. Leo jijini Dar es Salaam.

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisari Matiku Makori akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda  kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni. Leo jijini Dar es Salaam.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimkabidhi katiba na ilani ya chama cha mapinguzi (CCM) Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisari Matiku Makori mara baada ya kumwapisha leo jijini Dar es Salaam.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya wa mkoa wa Dar es Salaam,leo

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya jiji la Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemuapisha Kisari Matiku Makori kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni.

Akimuapisha Mkuu huyo wa Wilaya RC Makonda ameeleza kuwa wananchi wa Ubungo wanamatumaini na uteuzi wake na lengo kuu la kuanzisha wilaya ya Ubungo ni kusogeza huduma za wananchi karibu hivyo inabidi ahakikishe anatatua changamoto zao kwa kuwafuata huko waliko na asiridhike na ripoti anazoletewa ofisini kwani kumekuwepo na changamoto kubwa ya uwajibikaji hivyo inabidi hajiridhishe kwanza.

Katika hatua nyingine RC Makonda amewaagiza wakuu wa wilaya wote kutoruhusu wananchi kubomolewa nyumba zao mpaka kuwepo hukumu halali ya mahakama kwani wananchi wamekuwa wanaonewa na kudhulumiwa haki zao, hivyo wakuu wa wilaya kwa kushirikiana na jeshi la polisi wahakikishe haki inatendeka kwa kufuatilia ukweli na kujiridhisha kwa kuzikagua nyaraka husika.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya huyo Makori ameomba ushirikiano kwa viongozi wenzake ili aweze kutimiza majukumu yake kikamilifu na kuahidi kuwa atafanya siasa za kuleta maendeleo ili kila mwananchi anufaike na rasilimali zilizopo.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post