» »Unlabelled » Huyu hapa ndio msaidizi wa timu ya England

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Kocha msaidizi wa klabu ya Chelsea Steve Holland, ameteuliwa kuwa msaidizi wa kocha mkuu wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate.

Chama cha soka nchini England (FA) kimethibitisha uteuzi wa Holland ambaye aliwahi kufanya kazi na klabu ya Crewe Alexandra kuanzia mwaka 2007 hadi 2008 na baadae alikuwa kocha wa kikosi cha wachezaji wa akiba wa Chelsea kuanzia mwaka 2009 hadi 2011.

FA wamesisitiza kuwa Holland ataanza kazi mara moja, na atasaini mkataba wa kuitumikia timu ya taifa ya England jumla, ili kutoa nafasi ya kusaidiana kwa uhakika na bosi wake Southgate.

Steve Holland na Southgate walishawahi kufanya kazi katika kikosi cha timu ya taifa ya England chini ya umri wa miaka 21, hivyo inaaminiwa watafanikiwa kuleta mabadiliko.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post