» »Unlabelled » Kikao cha Halmashauri Kuu CCM Chafanya mabadiliko ya kimfumo na kimuundo

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Tuesday, December 13, 2016

Chama cha Mapinduzi CCM kimefanya mabadiliko kadhaa ya kimfumo na kimuundo, ikiwemo kuteua watendaji wapya katika Sekretarieti ya Taifa ya chama hicho, kufuatia watendaji wa awali kupewa majukumu mengine.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho bwana Nape Nnauye amewasilisha maazimio ya kikao cha Halmashauri Kuu NEC taifa ya chama hicho mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam kilichofanyika Ikulu jijini humo chinu ya Uenyekiti wa Rais Dk.John Pombe Magufuli.

Aidha, bwana Nape Nnauye amebaisha teuzi mpya kwenye Sekretarieti ya chama hicho zinazolenga kuziba nafasi za wajumbe wa awali ambao baadhi yao wameteuliwa kuwa mabalozi.

Miongoni mwa wajumbe wapya walioteuliwa ni Mkuu wa wilaya ya Ubungo bwana Humphrey Polepole ambaye anachukua nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho iliyokuwa ikishikiliwa na bwana Nape Nnauye.

Miongoni mwa masuala mazito yaliyoamuliwa na mkutano wa halmashauri kuu ya CCM ni kufanya uhakiki wa idadi ya wanachama,kuanzisha mfumo wa kadi za kielektroniki, kuondoa nafasi na vyeo ambavyo havitambuliki kikatiba, kupunguza idadi ya wajumbe kwenye vikao vya juu vya CCM, suala la wasaliti na hali ya kisiasa Zanzibar.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post