» »Unlabelled » Bodaboda wa Kigamboni waanza kudhibiti uhalifu

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

 Tuesday, December 13, 2016

CHAMA cha madereva wa bodaboda na bajaji wilaya ya Kigamboni, kimesema kuwa kimeamua kuweka utaratibu maalumu wa kudhibiti uhalifu kwa kuweka namba kwa kila bajaji ili kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Idan Ngongi alisema kwa sasa kumekuwepo na ongezeko kubwa la bajaji na bodaboda, hivyo utaratibu huo utasaidia kuimarisha ulinzi.

“Kulikuwa na bajaji nyingi zinakuja kufanya kazi usiku Kigamboni na wala hazikuwa za Kigamboni, hivyo tukaona hiyo inaweza kuwa chanzo cha uhalifu na sisi viongozi tukaamua kukaa na kuweka mikakati ya kwamba kila kituo kihakikishe kinaandika namba za bajaji zake ili kijulikane,” alisema.

Alisema, “katika kila kituo kuna namba ambazo zimeandikwa KGN ikimaanisha Kigamboni na kuna namba za bajaji ambayo inaonesha ni kituo namba ngapi na chini kuna jina la kituo.

Tulifanya hivyo ili kuzitofautisha bajaji, hivyo hata kama mtu atapanda atajua amepanda bajaji ya eneo gani labda ni ya Feri, Tungi, Mjimwema au Kisiwani”.

Alisema lengo la kugawa namba hizo ni kuzuia uhalifu kwa sababu matukio mengi yalikuwa yakitokea usiku na yalikuwa yakifanywa na bajaji ambazo hazijulikani zinatokea wapi, hivyo namba hizo zitadhibiti uhalifu.

“Abiria akipanda bajaji kwa sasa ataona namba ubavuni itakayokuwa wazi kwake na kujua bajaji ni ya eneo gani hata akifanyiwa uhalifu atajua aliyemfanyia uhalifu ni mtu wa wapi au anatoka kituo gani."
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post