NENO albino linamaanisha mtu mweupe, linatokana na neno la lugha ya kilatini ‘albus’ lenye maana eupe, likitumika katika kueleza hali ya kundi la viumbe hai ambao wana upungufu wa ukosefu wa rangi katika ngozi, macho na nywele.
Albino wana ngozi nyeupe, nywele nyeupe au nyekundu na macho ya kijivu au ya bluu, rangi ya ngozi zao huwa tofauti na watu wengine katika familia yao moja ambao hawana hali ya ualbino na huonekana nyeupe zaidi katika familia ya watu weusi. Kwa Kiswahili mtu mwenye upungufu huo huitwa zeruzeru, lakini baadaye ilionekana kama jina hilo lina unyanyapaa na ndipo likazaliwa jina ‘albino’ ambalo kimsingi si Kiswahili.
Katika siku za karibuni, jamaa za watu wenye ualbino nchini wanaona pia si sahihi kuitwa ‘watu wenye ulemavu wa ngozi’ wakiona kana kwamba jina hilo linapingana na ukweli kwamba pia wana ulemavu kwenye macho na nywele na hivyo wakataka waitwe ‘watu wenye albinism’.
Hata hivyo wataalamu wa Kiswahili wanasita kutumia neno hilo kutokana na kuchanganya lugha mbili kwa sababu ‘albinism’ inaweza tu kusemwa ‘ualbino’, neno linalotamkika Kiswahili zaidi. Watu wengi katika jamii wana ufahamu mdogo kuhusu chanzo cha ulemavu huu hadi watu kudhani kwamba eti kwa kuwa na ulemavu huo pekee kunasababisha utajiri ama mafanikio endapo utapata kiungo cha mtu huyo.
Ujinga kama huu uliwahi pia kuwapata Watanzania kudhani mwenye kipara anasabaisha utajiri ama hata ngozi ya binadamu na ndipo kukaibuka dhana ya uchunaji wa ngozi. Ni ukosefu huo wa elimu juu ya jambo hili unaochangia sana kuimarisha imani potofu zilizokithiri juu yao.
Watu wenye ualbino huwa hawana uwezo kabisa au kuwa na uwezo mdogo wa kuwa na rangi kwenye ngozi zao, nywele na macho kutokana na kukosa pigimenti zinazosababisha utengenezaji wa rangi katika ngozi, nywele na macho ziitwazo ‘melanini’.
Rangi ya ngozi ya mtu inategemea kiasi cha pigimenti hizo za melanini kilichopo mwilini mwake. Wataalamu wanasema kama mtu akizaliwa na upungufu ama bila melanini kabisa hupata madhara ya ukosefu au upungufu wa rangi. Kadhalika wanasema hali ya ualbino ni ya kurithi na hivyo inaweza kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto.
Watoto wengi wanaozaliwa na ualbino wazazi wao wana rangi ya ngozi, nywele na macho ya kawaida lakini huenda wakawa na kinasaba cha ualbino. Wataalamu wanasema kinasaba cha ualbino ni pigimenti dhoofu ambayo haiwezi peke yake kuonesha ualbino mpaka mtu awe nazo mbili kwa pamoja.
Kama wazazi wote wawili wana vinasaba vya ualbino na wote hawaoneshi ualbino kuna uwezekano wa kupata mtoto albino kati ya mtoto mmoja hadi wanne kutegemea idadi ya watoto watakaozaa. Albino wote hutofautiana kufuatana na kiasi cha milanini walichonacho,
wengine wanayo kwa kiasi kidogo, wengine nyingi na wengine hawana kabisa. Huko nyuma baadhi ya wanaume walikuwa wakiwakimbia wake zao wanapozaa mtoto albino, wakati ukweli unaweza kuwa ni mwanamume mwenyewe ndiye anaweza kuwa mwenye kurithisha vinasaba vya ualbino.
Kimsingi huo ni ujinga wa hali ya juu kwa sababu albino ni binadamu wa kawaida aliyepungukiwa tu melanini kiasi kwamba rangi ya ngozi yake haiwezi kutengenezwa na kuwa kama ya mtu mwingine aliyejaaliwa kuwa na pigimenti hizo.
Mbali na wazazi, katika jamii yetu bado kuna watu ambao pia huwaona albino kama watu tofauti na watu wengine na kuwakwepa na wengine huwavumishia mambo yasiyo ya kweli. Kutokana na mwili wao kutokuwa na uwezo wa kutengeneza rangi, watu wengi waliozaliwa na ualbino hupatwa athari ya mionzi ya jua ambayo huweza kuwaletea saratani ya ngozi na hivyo namna nzuri ya kumsaidia albino ni ni kumwepusha na kufanya kazi ama kutembea kwenye jua kwa muda mrefu.
Watu wenye ualbino pia huwa na uoni hafifu na hivyo wanahitaji pia zana za kuwasaidia kuona hususan miwani.
Mchora katuni mmoja aliwahi kuchora katuni yake inayowashangaa watu wanaodanganywa na waganga wa jadi, hususan wa Kanda ya Ziwa, kwamba viungo vya albino vinaleta utajiri. Alisema kama viungo hivyo vingekuwa vinatajirisha mtu au kuleta manufaa fulani, basi wazazi wa watoto albino wangekuwa wa kwanza kutajirika au hata albino wenyewe!
Ni dhahiri kwamba hakuna uchunguzi wa kisayansi ambao umeonesha faida yoyote inayopatikana kwa kuua albino isipokuwa imani potofu ambazo ziko katika fikra za watu wachache wenye uchu wa madaraka, mali na vitu vingine.
Kumekuwa na upotoshwaji mwingi sana katika jamii yetu kupitia kauli za waganga ambao wao wenyewe hawajiwezi kwa upande wa kipato. Kuna ambao wamekuwa wakidanganywa kwamba wanaweza kupona magonjwa kama Ukimwi kwa kujamiiana na mtu mwenye ulemavu wa ngozi ama mwingine.
Wapo pia wanaobaka watoto ama vikongwe kwa imani kwamba watapata utajiri. Albino ni binadam kama alivyo binadam mwingine ukitoa mapungufu ya kukosa melanini. Ni muhimu Watanzania tuondokane na kudanganywa huko.
Toka lini ulemavu wa mtu, kipara cha mtu, ngozi ama kingine kikawa sababu ya utajiri?
Kifungu cha 14 cha katiba ya Tanzania inaelekeza kwa ufasaha kuwa kila mtu ana haki ya kuishi na kulindwa utu wake katika jamii kwa msingi ya kisheria. Serikali kwa kushirikiana na taasisi na asasi za kijamii wanaendelea kutoa mafunzo, taarifa na mazingira yatakayowawezesha albino kuishi maisha yasiyo na hofu na hivyo kutoa mchango wao adhimu katika jamii.
Hawapaswi kuishi kwa hofu katika kijiji chao, mtaa wao au katika nchi yao. Jamii nzima na sisi sote mmoja mmoja na katika umoja wetu, tunao wajibu wa kuhakikisha usalama wa maisha yao na mali zao kama ilivyo kwa watu wengine wote,
Naamini ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na jamii utawezesha kutokomeza mauaji ya albino na kuliondolea taifa aibu hii.
Mauaji ya albino ni jambo linalofedhehesha na kulidhalilisha taifa na kwamba ni vitendo visivyovumilika na kwamba Serikali imelipa uzito mkubwa suala la kudhibiti na kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi au kukatwa baadhi ya viungo vyao wenyewe wakiwa hai.
Lakini ombi kwa mamlaka husika ni kwamba kutakapotokea mauaji ama albino kukatwa kiungo ni vyema polisi wahamie na kuweka kambi katika eneo hilo na kufanya operesheni kubwa katika kuhakikisha, si tu wahusika wanapatikana bali pia jamii inatishika.
IMETOSHA MAUAJI YA ALBINO