Zaidi ya wasichana 7,000 wa shule za msingi na sekondari mkoani Mwanza wamekatishwa masomo kutokana na sababu mbalimbali hasa kupata mimba za utotoni.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Pamba, Jijini Mwanza
Akizungumza katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambayo uhadhimishwa tarehe 25 ya kila mwaka duniani kote Mkurugenzi wa shirika la kutetea wanaweke KIVULINI Yasini Ally amesema takwimu nyingi zinaonesha katika mkoa wa Mwanza kumekuwa na changamoto kubwa kutokana na mazingira ya shule.
Pia ameyataja maeneo ya wavuvi hasa Sangabuye,luchelele,na kayenze wasichana wengi muda mwingi wa masomo wanakutwa wakiwa katika sehemu za starehe na gheto kama viburudishona wa wanaume na watu wanaona lakini wako kimya bila kuchukua hatua.
Hata hivyo bado takwimu hizo zinaonesha katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kuwa kinara kwa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia na kuongeza kuwa sasa wanahamishia nguvu yao katika wilaya hiyo ili kukomesha matukio hayo.