» »Unlabelled » El Hadji Diouf amkandia Steven Gerrard

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


El Hadji Diouf kwa mara nyingine tena amemkandia mchezaji mwenza wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard baada ya legend huyo kutangaza kustaafu rasmi soka.

1

Muingereza huyu ,36, ambaye alishinda taji la Ligi ya Mabingwa pamoja na matajai ya FA jana ametagaza kustaafu rasmi kucheza soka.

Diouf ambaye aliiumikia Liverpool kwa misimu miwili aliwahi kumkosoa Gerrard nyakati za nyuma na kwa mara nyingine tena amerudia kufanya hivyo.

“Wakati nilipowasili pale, nilimuonesha kuwa hakuwa chochote,” Diouf alisema.

“Nilimuuliza,’Ni michuano ipi mikubwa umecheza na watu ni sehemu gani hasa umeacha kumbukumbu kwa watu?’ Hakuwa Zinedine Zidane.

“Kama mchezaji, namheshimu sana. Ni mchezaji mkubwa. Lakini kama mtu ama binadamu wa kawaida hapana. Nilijitahidi kumfanya afahamu hilo.

“Kwangu mimi alikuwa mchezaji wa kawaida kama wengine tu. Alitakiwa ajiweke vizuri na kucheza kama ambavyo alifahamu aliutambua wajibu wake, lakini usiende kwa kocha na kuwachongea wenzako kuhusu yanayoendelea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.”

Diouf anaamini kwamba Gerrard alikuwa akimhofia sana, huku akiongeza: “Anajua vizuri kwamba simung’unyi maneno.

“Hakuwa akiniangalia machoni mwangu kwasababu alinihofia sana. Na zaidi alikuwa akihofia hata kuongea na mimi.

“Na nilipojiunga na Liverpool ni yeye ndiye alikuwa wa kwanza kuomba jezi yangu.”

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post