» »Unlabelled » Wanyama kulindwa kijeshi

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

KATIKA kukabiliana na ujangili, Wizara ya Maliasili na Utalii imetangaza kuanzisha mfumo wenye nguvu ya hadhi ya kijeshi ambao utalinda moja kwa moja wanyama wasishambuliwe na kuuawa na majangili.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali mstaafu Gaudence Milanzi alisema juzi jioni kuwa serikali imeajiandaa kuhakikisha inazuia ujangili na kwamba mkakati huo mpya una lengo la kumaliza kabisa tatizo hilo.

Alikuwa akizungumzia utendaji wa mwaka mmoja wa wizara yake kwenye kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Alisema watakaoshiriki kwenye kikosi hicho cha kijeshi watapata mafunzo ya nguvu ya kijeshi na watapewa silaha za kisasa kukabiliana na kupambana na majangili hao.

“Tunakwenda kuanzisha kikosi maalumu kitakachokabiliana na majangili, kitakuwa kikifuata mfumo wa kijeshi na watakuwa na silaha za kisasa,” alisema.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, kikosi hicho kipya kinatarajiwa kupambana ardhini ana kwa ana na majangili hao.

Alisema kwa kuwa Sekta ya Utalii inachangia asilimia 17.5 katika Pato la Taifa serikali inalazimika kutumia kila mbinu kulinda sekta hiyo. Kwa upande wa Utalii, Milanzi alisema wizara inafanya kila kitu katika uwezo wake kutangaza utalii nchini.

Alisema wizara pia imelenga kutangaza fukwe, mikutano na utamaduni wa kitalii.

“Sasa tunakwenda upande mwingine ili kuvutia watalii wengi zaidi, hivi sasa tutazitangaza fukwe, utamaduni pamoja na mikutano ya kitalii, lengo ni kuongeza idadi ya watalii wanaotoka nchini mwentu kuanzia milioni 1.1 hadi namba kubwa zaidi,” alisema.

Aliongeza kuwa wizara yake inatangaza sehemu nyingine za nchi ili watalii wawaweze kutembelea. Hadi sasa asilimia 80 ya watalii wanatembelea Kaskazini mwa Tanzania. Alisema wizara pia inaandaa matangazo maalumu ambayo yatarushwa kwenye vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post