» »Unlabelled » Hukumu TPA kuwa Januari

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imesema itatoa hukumu ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayowakabili vigogo wa zamani wa Mamlaka ya Bandari (TPA), akiwamo Mkurugenzi Mtendaji, Ephraim Mgawe na Naibu wake, Hamad Koshuma, Januari 6, 2017.


Hukumu hiyo ilipangwa kusomwa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Mfawidhi, Cyprian Mkeha lakini alisema bado haijawa tayari hadi mwakani.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Jaqckline Nyantori ulidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya hukumu.
Hata hivyo, hakimu alisema hukumu hiyo itasomwa Januari 6, na dhamana ya washtakiwa inaendelea.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya kwa kutoa zabuni kwa kampuni ya China Communication Construction Company Limited (CCCCL), kwa ajili ya ujenzi wa Gati namba 13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post