Idara ya upelelezi nchini Kenya yatoa ilani ya tahadhari kwa uwezekano wa wanamgambo wa Al Shabaab kupanga shambulizi katika pwani ya nchi hiyo.
Ripoti Ä°liyotolewa na idara hiyo ilibainisha mashambulizi ya kigaidi yanaweza kutekelezwa katika kaunti za Kilifi,Tana River na hata Kitui.
Hata hivyo hakukutolewa maelezo zaidi kuhusu taarifa hiyo.
Hata hivyo inasemekana kuwa kwanzia Novemba 7 kuna wanamgambo wanne waliowasili mjini Malindi na wanatumia gari aina ya Toyota Prado kupanga mashambulizi hayo.
Washukiwa hao wa ugaidi wanakisiwa kuingia nchini kutoka Somalia baada ya kupata mafunzo ya kijeshi.
Polisi nchini wamesambaza nambari ya gari wanalotumia kuzunguka nchini pamoja na vitambulisho vyao katika kila vituo vya ulinzi na usalama.
Hivi karibuni washukiwa 8 tayari wamekamatwa na polisi kutoka Malindi na msitu wa Boni.