Mji wa Jerusalem ni mojawapo ya maeneo 13 yaliyokumbwa na janga la moto mkali ambao ulianza siku ya Jumanne na unaendelea kuenea hadi kufikia sasa.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa ni kuwa moto huo umesababishwa na ukavu pamoja na upepo mkali ambao umekuwa katika kanda hiyo kwa muda wa miezi 2.
Msemaji mkuu wa polisi Micky Rosenfeld alifahamisha kuwa usiku wa kuamkia Ijumaa moto huo Jerusalem umeongezeka huku maeneo ya Hayfa kupungua .
Maelfu ya makaazi ya watu yameteketezwa huku hasara kuu pia kuripotiwa kutokea .
Shirika la msaada la msalaba mwekundu la Israel lilichapisha ripoti iliyoonyesha kuwa watu 70 wamepata majeraha madogo kutoka Hayfa .
Waziri mkuu Benjamin Netanyahu naye katika maelezo yake alisema kuwa chanzo cha moto huo ni shambulizi kutoka kundi la kigaidi.
Aidha Netanyahu alisema kuwa watakaopatikana na makosa ya kusababisha moto huo pia watapokonywa uraia .
Kulingana na taarifa kutoka vyanzo vya habari vya Israel ni kuwa mashirika ya wazima moto ya Filistina pia wameanza kutoa msaada wa kuzima moto katika Hayfa .
Vilevile Uturuki,Ugiriki na Italia pia tayari imetuma ndege Israel ili kusaidia katika shughuli ya kukabiliana na moto huo.
Siku ya Alhamis Netanyahu alituma ujumbe wa shukrani kwa Uturuki kwa msaada waliotoa .