» »Unlabelled » Tabia 3 Za Watu Wanaokubalika Sana Na Jamii

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Katika maisha bila shaka umewahi kuona watu wanaokubalika sana katika jamii yao. Kila ulipofatilia mienendo yao ulikuja kugundua kwamba watu hao kila wanaloligusa katika maisha yao ni kama linakubalika sana na wengi.

Pengine ilifika mahali ukajiuliza mengi kwa kuwaza na kusema “ Mmmh inawezekana watu hawa ni Freemason na sio bure kwa nini wao tu wanakubalika na sisi hapana?”.

Najua unayo mifano mingi ya watu kama hawa ambao wanakubalika sana na jamii. Je, ulishawahi kujiuliza ni kitu gani hasa ambacho kinasababisha watu hao waweze kukubalika kwa jamii kiasi hicho?

Majibu ya maswali hayo ya ni nini ambacho kinawafanya hadi wao wawe na mvuto mkubwa unakwenda kuyapata kwenye makala haya. Je, unataka kujua ni nini kinachofanya wawe ni watu wa kukubalika au wawe ni watu watu?

Hebu fuatana nami katika makala haya kujifunza baadhi ya tabia zinazowafanya wawe na mvuto.

1. Tabia ya kujenga tabasamu.
Tafiti nyingi zinaonyesha tabasamu ni kitu muhimu sana katika mahusiano yoyote yale yawe ya kimapenzi au kawaida. Kwa mfano, tabasamu huwa ni kichocheo cha kuwavuta wengi kusikiliza au kutambua umuhimu wa mtu anayetoa tabasamu hilo.

Pia tafiti hizo zinaendelea kuonyesha kila unapotasamu inasaidia kuwasisimua wengine kujaribu kukusikiliza. Hiyo ikiwa na maana kwamba hakuna mtu ambaye anapenda kumsikiliza mtu aliyenuna nuna. Ni lazima uwe na tabasamu fulani ili usikilizwe.

Kampuni nyingi zenye mafanikio kwa kujua hili, ndio maana zimeajiri watu wenye nyuso za bashasha au tabasamu pale mapokezi. Hivyo, Kama unataka kukubalika katika jamii, jifunze namna ya kutengeneza tabasamu zuri litakalo wavuta wengine kwako.

2. Tabia ya kusaidia wengine.
Mara nyingi watu wanao kubalika na jamii kwa sehemu kubwa, ukiwachunguza utagundua ni watu wa kusaidia watu wengine pia. Matatizo au changamto za jamii huyachukulia kama yao. Hivyo kila wakati hushirikiana na jamii zao kuweza kutatua yale yaliyo muhimu.

Kutokana na tabia hiyo ambayo wamejijengea, huwasaidia sana kuweza kuwa watu waliokubalika katika jamii kwa sehemu kubwa. Ni kitu ambacho hata wewe unaweza ukakifanya ili kuweza kuvuta mvuto kwa jamii yako hasa unayoishi.

3. Tabia ya shukrani.
Watu wanaokubalika na jamii na kupendwa na wengi maisha yao yametawaliwa na shukrani. Sio watu wazito sana kushukuru. Kila wanachokipata au pale wanaposaidiwa ni rahisi kwao kuweza kusema ansante mara moja.

Kwa kawaida shukrani yoyote haina gharama. Anza leo kujifunza kushukuru kwa mambo madogo madogo. Wape shukrani ndugu zako waliokutembelea au hata yule aliekupigia simu. Kwa jinsi utakavozidi kufanya hvyo itakusaidia kwako wewe uweze kukubalika kwa jamii yako.

Zingatia sana kwa kadri utakavyozidi kufanyia kazi tabia hizo, ndivyo utajikuta unakuwa ni mtu wa kukubalika na kupendwa na jamii yako kwa sehemu kubwa.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post