» »Unlabelled » Bil 16/- kukarabati barabara Singida

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

WAKALA wa Barabara mkoa wa Singida (Tanroads) inatarajia kutumia zaidi ya Sh bilioni 16.75 kugharamia ujenzi wa barabara zake mbalimbali mkoani hapa kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017.

Meneja wa Tanroads mkoa wa Singida, Leonard Kapongo alikiambia Kikao cha 38 cha Bodi ya Barabara mkoa kuwa kati ya kiasi hicho cha fedha, Sh bilioni 6.57 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara kuu wakati Sh bilioni 10.18 ni kwa matengenezo ya barabara za mkoa.

Alisema jumla ya kilomita 496.6 za barabara kuu zimepangwa kufanyiwa matengenezo ya aina mbalimbali kwa kipindi hicho, ikiwa ni pamoja na matengenezo ya kawaida, vipindi maalumu, sehemu korofi na ujenzi wa daraja moja kubwa Malendi mpakani mwa Singida na Igunga.

Kapongo alisema katika mpango wa matengenezo ya barabara za mkoa, jumla ya kilomita 796.6 na madaraja 36 yatahudumiwa, ikiwa ni pamoja na matengenezo ya kawaida, vipindi maalumu, sehemu korofi na madaraja makubwa saba na madogo 29 tu.

Aidha, Kapongo alisema kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha, waliweza kuandaa zabuni za kazi na kukamilisha kazi za viporo kwa mwaka wa fedha uliopita ambapo jumla ya kazi zenye thamani ya Sh bilioni 6.53 zimeandaliwa.

Kwa mujibu wa Meneja Kapongo, Wakala wa Barabara mkoa wa Singida inahudumia jumla ya kilomita 1,693.27 za barabara kuu na barabara za mkoa.

“Kati ya hizo, kilometa 476.6 ni barabara za lami, sawa na asilimia 28.2 na kilometa 1,216 (asilimia 71.8) ni za changarawe,” alisema.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post