» »Unlabelled » Zifahamu nchi 9 ambazo zinahimiza raia wake kuzaliana zaidi

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO
Kwa maendeleo ya nchi yeyote, rasilimali watu ni kitu cha muhimu sana. Ukiwa na miundombinu mizuri na hospitali nzuri kama nchi inaupungufu wa watu ni changamoto kubwa sana.

Tumeona nchi mbalimbali zimekuwa zikibadilisha sera za uzazi mara kwa mara lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na raia wa kutosha na wenye afya ya mwili na akili.

Kufuatia hatua hiyo, mataifa 9 duniani yamewashauri wananchi wake kuzaa watoto zaidi kutokana na upungufu wa watoto katika mataifa hayo.

9. Denmark

Denmark

Nchini  Denmark wananchi wake wameambiwa kuwa hata kama hawana mpango wa kuwa na watoto kwa ajili ya famili zao wenyewe, basi wazae japo kwa ajili ya nchi ili kuongeza idadi ya watu.

8. Urusi

Russia

Nchini Urusi wanaume wengi hufariki wakiwa vijana. Ugonjwa wa UKIMWI na  unywaji pombe kupindukia unasababisha vifo na hata kupoteza nguvu za kiume kitu kinachopelekea wanawake kushindwa kuzaa.

Tatizo hili lilikuwa kubwa kiasi cha mwaka 2007 Urusi kutangaza kuwa Septemba 12 ni siku ya kutafuta watoto. Siku hiyo wazazi hawaendi kazini na hubaki nyumbani kujamiiana ili kupata watoto. Atakayezaa mtoto baada ya miezi 9 toka siku hiyo anazawadiwa friji.

7. Japan

Japan

Japan imekumbwa na matatizo ya uzazi tangu mwaka 1975. Mwana 2010 wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Tsukuba walitengeneza roboti mtoto ambaye hupewa wazazi ambao hawana mtoto wakiamini kuwa wakikaa na roboti huyo kama mtoto watashawishika kupata mtoto wa kweli.

6. Romania

Romania

Miaka ya 1960 Romania ilikumbwa na tatizo la uzazi ambapo serikali ilifikia uamuzi wa kuweka kodi ya asilimia 20 kwa wapenzi wasio na mtoto na kuweka kifungu cha sheria kilichokuwa kikifanya utoaji talaka kuwa mgumu.

Hizi zote ni jitihada za kuhakikisha kuwa idadi ya watu inaongezeka.

5. Singapore

Singapore

Kutokana na upungufu  wa watu nchini Singapore, serikali ya nchi hiyo imeweka vizuizi kwa nyumba za kulala wageni au hoteli kuwa na vyumba vingi vya kulala mtu mmoja mmoja. Hi ni kuta kuwepo ongezeko la watu kuweza kulala wawili wawili.

Serikali ya Singapore hutumia takribani dola bilioni 1.6 kwa mwaka katika kuhakikisha kuwa watu wanajamiiana sana ili kuongeza idadi ya watu.

4. Korea Kusini

South Korea

Kila Jumatano ya tatu ya kila mwezi, ofisi nchini Korea Kusini huzima taa zake saa 1:00 usiku ambapo siku hiyo hufahamika kama Siku ya Familia.

Pia serikali ya nchi hiyo hufanya kila njia kuhakikisha kuwa kunakuwepo na ongezeko la watu ikiwa ni pamoja na kuwalipa watu ambao watazaa mtoto zaidi ya mmoja.

3. India

India


Nchi nzima ya India kwa ujumla haina upungufu wa wa watu. Lakini watu wa jamii ya Parsis wanapungua kwa kasi. Watu wa jamii hiyo wamepungua kutoka 114,000 mwaka 1941 hadi 61,000 mwaka 2001.

Kufuatia hali hiyo, serikali ya India imekuwa imkiwataka watu wa jamii hiyo kutotumia mipira ya kiume au ya kike (condoms) wakijamiiana usiku. Pia imeendeshwa kampeni ya kutaka vijana kujitegemea na kuacha kuishi na wazazi wao. Hii imechangia kuongezeka kwa watu hadi 69,000.

2. Italia

Italy

Kama ilivyo kwa nchi nyingine, Italia nayo imeedesha kampeni mbalimbali kushawishi raia wake kuzaa watoto zaidi. Lakini kampeni hizo zinaelezwa kutozaa matunda.

1. Hon Kong

Hong Kong

Tofauti kidogo na nchi nyingine, Hon Kong ina wazee wengi na upungufu wa vijana na watoto. Hii ni hatari kwa uchumi wa nchi hiyo baada ya wazee hao kufariki.

Mwaka 2013, nchi hiyo ilianzisha kampeni kwa kuwalipa fedha wanandoa ambao wanazaa watoto. Serikali inalipa dola 4,440 kwa mtoto wa kwanza na wa pili na dola 5,900 kwa mtoto wa tatu na wanne. Mpango huu Hong Kong iliuchukua kutoka Singapore.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post