» »Unlabelled » Wahofia mafuriko darasa la kwanza

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Bukombe. Idadi ya wanafunzi wanaotarajiwa kuandikishwa kuanza darasa la kwanza na elimu ya awali katika Kata ya Bulangwa wilayani Bukombe mkoani Geita huenda ikaongezeka kutoka asilimia 60.4 ya mwaka huu hadi  81 kutokana na mwamko wa wazazi.

Mratibu Elimu Kata ya Bulangwa, Dunkani Ruzige aliimbia Mwananchi juzi kuwa mwaka huu, zaidi ya wanafunzi 1,863 waliandikishwa katika shule zilizoko kwenye kata hiyo, idadi inayotarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 20 mwakani.

“Wazazi wengi wamepata mwamko wa kuwaandikisha watoto wao hasa baada ya Serikali kuanza kutekeleza Sera ya Elimu ya Msingi Bure,” alisema Ruzige.

Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Mariko Nsoro aliwataka wazazi na walezi wanaotarajia kuwaandikisha shule watoto wao kufanya maandalizi mapema kwa kuwanunulia sare na mahitaji mengine kama madaftari na kalamu.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post