Msajili wa Hazina Bw. Lawrence Mafuru amewataka viongozi wa mashirika na taasisi za umma zilizopo chini ya ofisi yake kuwajibika kwa kuhakikisha mashirika yao yanaongeza ufanisi kwa mujibu wa matarajio ya serikali .
Mafuru pia ameyaeleza mashirika hayo kuwa kushindwa kufanya hivyo ni ishara kwamba viongozi hao hawastahili kuendelea na nyadhifa zao.
Bw. Mafuru ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam katika mahojiano na EATV na kusisitiza kwamba kamwe ofisi yake haitovumilia utendaji wa kimazoea ambao kwa muda mrefu umeyafanya mashirika ya umma kuwa tegemezi wa ruzuku kutoka serikalini huku yakiendelea kupata hasara mwaka hadi mwaka.
Aidha, Msajili huyo wa Hazina hakusita kuzungumzia tatizo sugu la ulimbikizaji madeni na hapa ameziagiza taasisi zote kulipa madeni wanayodaiwa kutokana na huduma walizotumia kutoka taasisi nyingine za umma na kwamba kuna haja ya taasisi hizo kuwa na mtazamo wa kuziendesha taasisi zao kama yalivyo mashirika ya umma.