
Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi katika ukumbi wa Maisha Basement, Snura amesema kuwa video hyo imeruhusiwa kutoka kutokana na makubaliano waliyoyafanya tangu alipofungiwa kua kama anataka wimbo huo uchezwe basi aufanyie marekebisho.
Aidha, akieleza maana ya neno chura katika wimbo wake, amesema kuwa chura anayemzungumzia yeye ni mwanamke ambaye hajatulia katika mahusiano na kuwa ana tanga tanga kwa wanaume mbalimbali.
Katika barua ya Waziri Nape, amemuonya Snura kutorudia tena kufanya video au kuimba kitu ambacho kipo kinyuma na maadili ya Tanzania.
