Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba wameingia uwanjani na kuwasalimu mashabiki uwanjani hapo.
Mashabiki wa Yanga muda mwingi wameonekana kuwa wapole tofauti na wapinzani wao Simba ambao wameonekana wakishangilia kwa nguvu muda wote.
Simba ilikuwa ya kwanza kuingia uwanjani kufanya mazoezi wakiongozwa na makipa wake Peter Manyika na Vincent Angban walionza kufanya mazoezi uwanjani. Yanga ilifuatia kwa kutoka wachezaji wote Saa 9:15 wakiongozwa na Amissi Tambwe.
Katika mchezo wa timu za vijana uliochezwa mapema Yanga B ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba B. Ushindi huo wa Yanga B ulipokelewa kwa nguvu nyingi na mashabiki wa Yanga.