» »Unlabelled » Serikali mkoani Mwanza imezionya hili Kampuni zinazotoa huduma ya usafiri wa Meli na vivuko ndani ya Ziwa Victoria

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Serikali mkoani Mwanza imezionya Kampuni zinazotoa huduma ya usafiri wa Meli na vivuko ndani ya Ziwa Victoria, kutozidisha uwezo wa kubeba wa mizigo ili kulinda usalama wa abiria na mali zao, katika Ziwa hilo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela, ametoa onyo hilo wakati akizindua Meli ya Mv. Nyehunge II katika bandari ya Kirumba, inayomilikiwa na Kampuni ya Mohamed and Brothers enterprises, itakayokuwa ikitoa huduma ya usafiri kati ya Mwanza na Kisiwa cha Ukerewe.

Kuzinduliwa kwa Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 500, magari na mizigo, kutapunguza kero ya usafiri iliyokuwa ikiwakabili wakazi wa kisiwa hicho, hatua ambayo imekuwa ni faraja kwa abiria wanaotumia usafiri wa majini kati ya Jiji la Mwanza na Kisiwa cha Ukerewe.

Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Mohamed and Brothers enterprises, Said Mohamed, akazungumzia Mv. Nyehunge II itakavyoboresha huduma ya usafiri, ili kuondoa adha ya ukosefu wa huduma hiyo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa Kampuni ya Mohamed and Brothers enterprises, kivuko hicho cha Mv. Nyehunge II kitakachotatua tatizo la uhaba wa vyombo vya majini mkoani Mwanza, kimegharimu zaidi ya shilingi milioni 800.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post