» »Unlabelled » Serikali kuthamini ubunifu wa kutunza mazingira

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),  Janaury Makamba amesema Serikali itaendelea kuthamini ugunduzi na ubunifu unaosaidia kupunguza athari za mazingira kwa manufaa ya Taifa.

Makamba ametoa kauli hiyo wakati leo alipotembelea kikundi  cha Kuja na Kushoka kilichopo Kata ya Kiloleni kinachozalisha mkaa mbadala ili kuzuia ukataji wa miti inayotumika kutengeneza mkaa na kuni pia.

"Ubunifu huu wa kikundi hiki utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi ukataji wa miti kwa ajili mkaa na kuni unaosababisha uharibifu wa mazingira kwa mkoa wa Tabora na nchi nzima kwa ujumla, "alisema Makamba

Meneja wa kikundi hicho, Lenard Kushoka alimweleza Makamba kuwa mbali na kutengeza mkaa mbadala pia watengeneza majiko banifu kwa ajili ya kukaushia tumbaku ambayo ni zao biashara mkoani humo.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post