Wananchi wa jamii ya Kimasai katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wamekumbwa na hofu ya usalama wa maisha yao baada ya kuzuka kwa wimbi la majangili ambao wamevamia makazi ya wananchi wa kijiji cha Ngage na kuua Punda zaidi ya 70 na kisha kuwachuna ngozi nyakati za usiku.
Wakizungumza kwa masikitiko wananchi hao wamesema tangu kuzuka kwa wizi wa Punda miezi miwili iliyopita wananchi wa jamii ya kimasai wanaishi kwa hofu kubwa kwa kuwa wanategemea wanyama hao kama vyombo vyao vya usafiri na kuwasaidia kubeba mizigo.
Kufuatia tatizo hilo wananchi hao wamesema wanahofu kubwa kwa kuwa watu hao wanavamia maboma ya wamasai nyakati za usiku wakiwa wamelala na kuiba Punda hizo na kuzichinja na kisha kuondoka na ngozi jambo ambalo wanasema hawajawahi kuona matukio hayo ambayo yamezuka tangu mwezi Agusti mwaka huu.
Diwani wa kata ya Loibosort Mh.Simon Kikoda amekiri kuwapo kwa wizi wa Punda na kwamba tatizo hilo linawaathiri zaidi wanawake ambao ndiyo wanatumia zaidi usafiri wa Punda kutokana na kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji safi pamoja na kusafirisha mizigo kuuza na kununua kwenye minada.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Simanjiro Mh. James Ole Milya ameliomba jeshi la polisi kudhibiti ujangili huo ambao unawaathiri wafugaji wa jamii ya kimasai na kwamba wizi huu umekuja siku chache baada ya kufunguliwa kwa kiwanda cha Punda katika mkoa wa Dodoma.