» »Unlabelled » Pambano la ndondi kati ya Cheka na Debeman laota mbawa

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Pambano la ndondi la kimataifa kati ya Mtanzania Cosmas Cheka na Jason Debeman, raia wa Afrika Kusini limeingia dosari baada ya Debeman kugoma kupanda ulingoni usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Pambano hilo la raundi 10 la uzito wa kilogramu 64 limebadilisha mtizamo wa mamia ya mashabiki waliojitokeza kulishuhudia.

"Siwezi kupigana na sitofanya hivyo.” Ilikuwa kauli ya Debeman akisisitiza kutozichapa kwenye pambano hilo akisema alisaini mkataba ili kuzichapa na Ibrahim Class na si Cheka.

Mashabiki waliojitokeza kwa wingi Diamond Jubilee sasa wanalazimika kushuhudia pambano kati ya Dulla Mbabe na raia wa China, Chengbo Zheng.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post