
Ni wajibu wako mfanyakazi pia kuhakikisha unamkumbusha mwajiri wako kufanya hivyo na/au ikishindikana waweza kumchukulia hatua.
JE? NI KOSA LA JINAI KUTOMSAJILI MWAJIRIWA KATIKA MFUKO WA HIFADHI.
Kwa mujibu wa Mwanasheria na msahauri wa Gazeti la serikali la Habari Leo Bashir Yakub amefanunua jambo hilo kuwa ukisikia makosa ya jinai ni yale makosa ambayo mtu hushitakiwa na Jamhuri. Ni makosa ambayo mnatendeana wawili lakini anayeshitaki ni Jamhuri/Serikali. Ni makosa ambayo ukipatikana na hatia adhabu zake huwa ni vifungo, faini na wakati mwingine kuchapwa bakora. Kwa maana hii mwajiri yeyote ambaye amekataa kumsajili mfanyakazi wake katika mfuko wa hifadhi ya jamii anakuwa ametenda kosa la jinai ambapo anastahili kuadhibiwa.
Kosa hili limeingizwa katika makosa ya jinai kutokana na umuhimu wa mifuko hii. Lakini pia ni kutokana na ukweli kuwa waajiri wengi wasingependa kuwasajili waajiriwa wao kwa kuwa wao hutakiwa kuchangia asilimia kadhaa ya fedha kila mwezi. Kwa kuwa wasingependa wachangie fedha hizi ndio maana ikaingizwa kwenye jinai ili wa kuogopa na aogope.
