
MKURUGENZI WA TPA, DEUSDEDIT KAKOKO.
Hali hiyo imejidhihirisha kutokana na taarifa kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) haikuhusishwa vya kutosha katika utoaji wa taarifa sahihi juu ya suala hilo huku TBS wakidai kuwa hadi kufikia jana, tayari wafanyabiashara 10 walishajitokeza kwao kwa nia ya kutoa maelezo.
Akiwasiliana na Nipashe jana, Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, alielezea kushangazwa na taarifa zilizoelezwa kuhusiana na kontena hizo.
Aidha, Kakoko alisema hali hiyo ya kutolewa maelezo bila kutaka taarifa kwao ni sawa na ‘kukwepa kupata taarifa sahihi kutoka sehemu sahihi’.
Source: nipashe
