» »Unlabelled » Diwani na mkewe kizimbani

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Sumbawanga. Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa, linamshikilia Diwani wa Kata ya Izia (Chadema) na mkewe kwa tuhuma ya kukutwa na bunduki aina ya gobori na dawa za kulevya aina ya bangi kinyume na sheria.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, George Kyando amesema watuhumiwa hao wamekamatwa i dukani kwao katika eneo la soko kuu, Kata ya Mazwi, Manispaa ya Sumbawanga  kwenye msako uliokuwa unaendeshwa na askari wa jeshi hilo.

Taarifa za kipolisi zilieleza kuwa msako huo ulifanyika baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba watuhumiwa hao wanamiliki silaha.

Kyando alisema silaha hiyo na bangi yenye uzito wa robo kilo vilikutwa vimefichwa  katikati ya mifuko ya ‘sulphate’.

Amesema watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa na polisi walikiri kukutwa na  vitu hivyo na watafikishwa mahakamani wiki ijayo baada ya upelelezi kukamilika.

Alitoa rai kwa wananchi kuepuka kujihusisha na uhalifu na kumiliki silaha isivyo halali.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post