» »Unlabelled » Serikali yakabidhiwa ndege zisizo na rubani kudhibiti ujangili

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Dar es Salaam. Shirika la Wanyamapori Duniani (WWF) limeikabidhi serikali ndege nane zisizo na rubani (drones) zenye thamani ya Sh 60 milioni kwa ajili ya kupambana na ujangili.

Ndege hizo zitawekwa katika mbuga na hifadhi ili kuchukua picha katika maeneo mbalimbali na kurudisha majibu.

Mwakilishi Mkurugenzi WWF nchini Meneja Uhifadhi Simon Lugangu amesema  ndege hizo zisizo na rubani zitachukua picha, kisha kuzihifadhi katika kompyuta  na  zitawasaidia askari wa maliasili kupata taarifa za majangili.

Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Majangili Kanda ya Kusini, Joshua Mmari  alizungumzia kupungua kwa tembo nchini na kusema  katika kipindi cha miaka ya 1970  kulikuwa na tembo 110,000 lakini  hadi 2014 idadi yao ilipungua na kubaki 15,000.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post