» »Unlabelled » Nyoka atafuta' joto' kwenye kiatu Australia

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Nyoka mwenye sumu kali atafuta 'joto' kwenye kiastu Australia

Mwanamke wa Australia amewaita maafisa wa wanyama pori kumtoa nyoka wa urefu wa mita 1 mwenye sumu kali kutoka kwenye kiatu chake.

Mnasa nyoka Rolly Burrell alimdhibiti nyoka huyo wa rangi ya chokoleti aliyekuwa anatafuta ''joto'' nyumbani mwa mwanamke huyo Adelaide, kusini mwa Australia.

Alikuwa ametoka nje ya nyumba yake iliopo mashambani kukusanya viatu vyake na hapo akaona mkia ukipotea ndani ya kiatu chake kimoja.

Nyoka huyo ni mmoja wa wanaoonekana kuwa wenye sumu kali duniani na hupatikana katika pwani na maeneo ya ndani ya ardhi kavu Australia.

Alitoka nje kuchukua viatu vyake na akaona kitu kikitoweka kwa kasi,

Rolly Burrell, Mnasa Nyoka

"Alitoka nje kuchukua viatu vyake na akaona kitu kikitoweka kwa kasi," Burrell ameiambia BBC.
"Aligundua kuwa ni nyoka."

Nyoka huyo ambaye ni aina inayopenda kujificha, alichiliwa msituni kando na mbali na maenoe ya makaazi ya watu .

Bwana Burrell amesema kampuni yake iliitwa kwa mara nyengine kutoa nyoka kwenye kiatu takribana mwaka mmoja uliopita.

Viatu hivyo aina ya buti, vimetengenezwa kwa ngozi ya kondoo, na hutumika sana Australia,
Huwana joto zuri wakati wa msimu wa baridi, pengine ndio sababu iliomvutia nyoka huyo.

"Ndio wanaanza kuamka kutoka usingizini," Bwana Burrell anasema.

"Msimu wao wa kujamiiana umeanza kwa hivyo wanatafuta joto na wana njaa."
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post