» »Unlabelled » Nilichokishuhudia kimenipeleka kuokoa maisha ya wahamiaji na wakimbizi

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Mimi na familia yangu tuliguswa sana na majanga yanayotokea katika pwani ya mediterenia na ndipo tukaamua kuchangia katika kuokoa maisha. Hayo ni maneno ya Christopher Catrambone, Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali linalokoa wahamiaji katika bahari ya mediterenia(MOAS).

Christopher na familia yake kwa miaka miwili sasa wameokoa maisha ya zaidi ya wahamiaji 27,000, kupitia shirika lao lisilo la kiserikali, ambapo ameieleza Radio ya Umoja wa Mataifa kilichomsukuma kuanza kazi hii.

“Nafikiri kuona na kushuhudia pande mbili hizi- na ni wazo ambalo hatujawahi kulifikiri- tukiwa likizoni ndani ya meli ya anasa, tulitambua na kujiuliza kuwa, sehemu hii ambayo sisi tunaifurahia , watu wanapoteza maisha yao”.
Amesema chuki dhidi ya wahamiaji na wakimbizi itatokomea endapo kila mkazi wa dunia atajihusisha nao kwa karibu zaidi, ili kupata uelewa wa maisha halisi ya kundi hili.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post