» »Unlabelled » Watuachie muziki wetu wafanye kiki zao- Mwana FA

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Msanii wa muziki wa Hip Hop Tanzania Mwana FA amefunguka na kusema kwenye muziki wa bongo sasa kumekuwa na wimbi kubwa la wasanii kufanya muziki kwa kutumia kiki katika mambo mbalimbali.

Amesema jambo hilo amekuwa akilipinga na kutofautiana nao kwa hilo kwani yeye anaamini kuwa muziki mzuri hauhitaji kiki kwa kuwa muziki mzuri unaongea wenyewe.

Mwana FA alisema haya kupitia kipindi cha Friday Night Live na kuwataka wasanii wanaofanya muziki kwa kutumia kiki waachaane na muziki na waendelee kiki zao ili wasiharibu muziki kwani anadai muziki mzuri hautaji kiki zozote zile.

"Mimi nipo tofauti sana mimi ni shabiki wa kwanza wa kazi zangu na siku zote nafanya kazi ili niwe bora sijui kwa wanamuziki wengine, lakini huwa napishana na watu wengi sana kwenye haya masuala ya kiki, muziki mzuri hautaji kiki. Saizi kuna wasanii wengi wa muziki, filamu wao kazi yao ni kutengeneza kiki ili kazi zao ziende mimi nasema watuachie muziki wetu waendelee kufanya kiki zao" alisema Mwana FA

Mbali na Mwana FA, aliyekuwa meneja wa mwanamuziki Ommy Dimpoz, Mubenga naye aliungana na Mwana FA na kusema ni bora hao wasanii wanaofanya muziki kwa kutegemea kiki wawaachie muziki mzuri na wao waendelee na maisha ya kutafuta kiki.

Kwa upande wake Professa Jay alisema kuwa kitendo cha wasanii kutegemea kiki kwenye kazi zao kinapelekea wasanii hao kila siku kutoa kazi mpya, sababu watu wanafuatilia sana kiki zao kuliko hata kazi zao.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post