
Baadhi ya wana hip hop wanadai kuwa Nay wa Mitego hafanyi hip hop halisi, lakini rapper huyo controversial amepata shavu ambalo hakuna msanii wa hip hop Bongo amewahi kulipata – kupewa shavu na rapper mkongwe, Snoop Dogg.
Haijulikani ameipata wapi video hiyo, lakini Snoop ameipost kwenye akaunti yake ya Instagram yenye followers zaidi ya milioni 11.8.
Ndani ya saa 18, video hiyo imepata views 486k na comments 1850.
Snoop aliandika kwenye video hiyo, “Jump jump jump jump.”
Nay ameirepost na kuandika: Mjomba @snoopdogg ametisha sanaaa nadhani Beat na Michano imemkumbusha mbaliii. OldSkul ndani ya NewSkul..! Inaenda mbaaaliiiiii #GoodTime
Bahati mbaya tu kwa Nay ni kwamba followers wengi wa Snoop hawajui kama ni yeye ndiye mwenye wimbo … laiti kama angemtag!
