» »Unlabelled » Samatta kuivaa Lokomotiva Zagreb, Europa League

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Shirikisho la Soka Barani Ulaya UEFA, limetangaza droo ya hatua ya mtoano ya ligi ya Ulaya ijulikanayo kwa jina la Europa League ambapo jumla ya vilabu 44 vitapambana ili kupata vilabu 22 vitakavyotinga hatua ya makundi ya ligi hiyo.

Katika droo hiyo klabu ya KRC Genk anayokipiga nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Mbwana samatta, imepangwa kukutana na Lokomotiva Zagreb (CRO) ya nchini Croatia.

Genk imefikia hatua hiyo baada ya jana kuiondosha Cork City ya Sweden kwa jumla ya mabao 3-1, ambapo ilipata ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kwanza na katika mchezo wa marudiano uliopigwa usiku wa kuamikia leo imeondoka na ushindi wa mabao 2-1 ikiwa ugenini.

Hicho ni kigingi cha mwisho kwa nyota huyo wa kitanzania alipitia vilabu vya Simba Sc ya Dar es salaam na TP Mazembe ya DRC kabla ya kujiunga na klabu hiyo katikati mwa msimu uliopita, kushiriki hatua ya makundi ya ligi ya Ulaya.

Kwa upande wa England, West Ham United imepangwa kukutana Astra Giurgiu ya nchini Romania.
Mechi za kwanza zitachezwa Agost 18 na kurudiana Agost 25. Timu 22 zitakazofuzu zitaingia katika hatua ya makundi zikiungana na timu nyingine 16 zilizofuzu moja kwa moja pamoja na nyingine 10 zitakazoondoshwa kutoka katika ligi ya mabingwa (UEFA Champions League.

Droo ya kupanga makundi itafanyika Agost 26, Monaco nchini Ufaransa.

Droo iliyofanyika leo imehusisha timu 29 zilizofuzu kutoka raundi ya 3 ya michuano hii, pamoja na timu nyingine 15 zilizotolewa katika ligi ya mabingwa
Matokeo ya droo iliyofanyika leo iko kama ifuatavyo:-
Astana (KAZ) v BATE Borisov (BLR)
AEK Larnaca (CYP) v Slovan Liberec (CZE)
Arouca (POR) v Olympiacos (GRE)
Dinamo Tbilisi (GEO) v PAOK (GRE)
Midtjylland (DEN) v Osmanlıspor (TUR)
Austria Wien (AUT) v Rosenborg (NOR)
Trenčín (SVK) v Rapid Wien (AUT)
Beitar Jerusalem (ISR) v Saint-Étienne (FRA)
Lokomotiva Zagreb (CRO) v Genk (BEL)
Vojvodina (SRB) v AZ Alkmaar (NED)
Maribor (SVN) v Qäbälä (AZE)
Gent (BEL) v Shkëndija (MKD)
Slavia Praha (CZE) v Anderlecht (BEL)
İstanbul Başakşehir (TUR) v Shakhtar Donetsk (UKR)
Astra Giurgiu (ROU) v West Ham United (ENG)
SønderjyskE (DEN) v Sparta Praha (CZE)
Fenerbahçe (TUR) v Grasshoppers (SUI)
Sassuolo (ITA) v Crvena zvezda (SRB)
Brøndby (DEN) v Panathinaikos (GRE)
IFK Göteborg (SWE) v Qarabağ (AZE)
Krasnodar (RUS) v Partizani Tirana (ALB)
Maccabi Tel-Aviv (ISR) v Hajduk Split (CRO)

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post